Friday, April 13, 2012

Je, ulipata matayarisho ya kuwa mama?

Habari mama. na uliye mama mtarajiwa.

Kuna msemo wa kiswahili unaosema kuzaa si kazi, kazi ni kulea. Bila shaka hata wewe umewahi kuusikia. Bila shaka unautumia mara kwa mara. Leo ningependa kukuliza. Je, unadhani kwa nini kulea ni kazi?. Sitegemei kupata jibu la moja kwa moja kwani hata mimi natambua kuwa kulea ni kazi. Tena kubwa sana. Ninatambua. Lakini kinachonisukuma leo hii kukuraibisha uchangie nami mawazo katika hili ni utashi wa kutaka kufahamu. Je, huwa tunaandaliwa kuwa mama? Tujadili tafadhali.



Wednesday, March 23, 2011